Posts

Showing posts from August, 2018

ISOME HII ITAKUSAIDIA SANA

*TUMIA DAKIKA 3 KUSOMA HII* Lameck alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana. Mara akakutana na akina Mama watatu ambao walinyoosha mkono kumuomba lift. Ingawa alikua na haraka lakini aliwaonea huruma na kusimama, sehemu waliyokuwa ilikuwa ni kichakani na kwakuwa alikuwa peke yake hakuona sababu ya kuwanyima lift. “Samahani Baba, tunaomba utusaidie tunaelekea, Usangi kwenye msiba sasa tumechelewa na magari hamna…” Mama mmoja aliomba. Lameck aliwaambia waingie kwani hata yeye alikuwa anaelekea huko huko. Wale akina mama waliingia kwenye gari aliwasalimia na bila hata kuulizwa walianza kujielezea. “Tunaenda kwenye msiba, kuna Mama mmoja kafariki huko...” Mama mmoja alianza kuongea na mwingine aliendelea… "...Ahsante sana mwanangu, ni vijana wachache sana wenye roho nzuri kama wewe, wenzako wametupita kama sisi sio watu, magari mazuri kama haya yenu hata hayasimamagi. Huko tunakoenda kuzika huyo Mama wa watu kaumwa kateseka lakini mtoto wake mwenyewe...